Tim Tibow ni balozi mzuri wa Bwana Yesu!

Tibow akiongea siku ya Pasaka

Akiomba uwanjani

Mchezaji wa American footbal (NFL) Tim Tibow ambaye amekuwa gumzo kwa wamarekani kwa style yake ya kupiga goti na kuomba bila kuogopa yeyote na hatua hii imemfanya kuweza kushinda mipira dakika za mwishoni.

Pamoja na umaarufu huo amekuwa akisema wazi kwamba yeye hawezi kuacha kumshukuru Bwana Yesu kwa kuwa yeye ndiye humshindia na hivi karibuni alibandika mstari maarufu kwenye uso wake Yohana 3:16 ambapo wamarekani wengi waliugoogle kujua maana ya mstari huo.

Ibada ya Pasaka alihudumu kwenye kanisa la Celebration Church kwa pastor Joe Champion, ambapo Tibow alihubiria umati uliofika kumsikiliza kwamba ni vizuri kuelezea kuhusu imani ya Kikristo na hata kuwa muombaji pia wanamichezo ni mfano bora wa kuigwa. Alipoulizwa kitu gani kinahitaji kubadilika Marekani, akajibu nchi kuwa chini ya Mungu.

Tibow tarehe 21 alinunuliwa na team ya New York Jets akitokea Denver Broncos, ambapo yeye anaona ni Mungu anazidi kumweka utukufu hadi utukufu.

Tim Tibow amekuwa akimuweka Yesu mbele, pamoja na changamoto anazopata kutokana na Imani yake kwa Bwana Yesu. Amekuwa ni mfano wa Kuigwa!

Advertisements

2 thoughts on “Tim Tibow ni balozi mzuri wa Bwana Yesu!

  1. Margareth,

    Nakubaliana na wewe, bila kuwa na watu kama Tim Tibow katika nyanja mbali mbali za Waamerika nadhani taifa hili lisingefika hapa lilipo, Kitu kikubwa ambacho nakiona Marekani ni kuwa walioamua kumtafuta na Kumuishia Mungu wameamua hasa……na walioamua kumuasi Mungu nao wameamua hasa……….

  2. hao ndio wanaoituliza hasira ya Mungu , hivyo Mungu kuinusuru nchi ya America. Mungu amshindie na ampe nguvu katika kuuinua utukufu wake amen.

Andika maoni yako

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s